MATANGAZO YA PAROKIA
1. Jumapili ijayo itakuwa Dominika ya Ishirini ya Kipindi cha Kawaida, Mwaka A. Tunawashukuru wote waliohudumu wiki hii. Huduma za Misa wiki ijayo:
* Misa ya Saa 12:30 asubuhi – C.J.P.D. Misa ya Saa 5:30 asubuhi – Mt. Anna
* Misa ya Saa 2:00 asubuhi – Senior Youth Misa ya jioni Saa 11:30
* Misa ya Saa 3:30 asubuhi – OLF Men
2. Siku za Watakatifu Juma hili:
* Jumatatu, 10/08/2026: Sikukuu ya Mt. Laurenti, Shemasi na Shahidi.
* Jumanne, 11/08/2026: Kumbukumbu ya Mt. Klara, Bikira.
* Ijumaa, 14/08/2026: Kumbukumbu ya Mt. Maksimiliano Kolbe, Padri na Shahidi.
* Jumamosi, 15/08/2026: Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni kwa Bikira Maria.
3. MCHANGO WA UJENZI WA GROTTO. Alhamisi, tarehe 13/08/2026, itakuwa siku ya mchango kwa ajili ya ujenzi wa Grotto. Tutasali Rozari saa 6:30 mchana ikiongozwa na wanakarama. Mchango utafanyika baada ya Rozari na jioni kwa Krusedi. Tunaombwa kuchukua bahasha.
4. KONGAMANO LA WIKI YA NEEMA (CRUSADE) linaanza leo, tarehe 09/08/2026, hadi tarehe 16/08/2026. Kutakuwa na mafundisho kila siku kuanzia saa tatu asubuhi, na mkutano wa Crusade saa tisa alasiri. Hakutakuwa na jumuiya mitaani wakati wa Crusade.
5. SEMINA YA VIJANA. Tarehe 13/08/2026 tutakuwa na semina ya vijana wenye umri wa miaka 13 na kuendelea, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana. Karibuni vijana wote. MADA: Vijana wa leo, Kanisa la kesho.
6. SEMINA YA WATOTO. Tarehe 14/08/2026 tutakuwa na semina ya watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 12, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana. Wazazi tunaombwa kuwasaidia watoto wafike. MADA: Watoto ni zawadi kwa wazazi wao.
7. HUDUMA ZA MATIBABU. Jumapili ijayo, tarehe 16/08/2026, shirika la Greenworld/Green Health International litatoa huduma za matibabu kwa njia ya virutubisho kwa maradhi kama maumivu ya mgongo, vidonda vya tumbo, ugumba kwa wanawake na wanaume, pumu, kisukari, shinikizo la damu, kizunguzungu na uchovu wa kila mara, na kadhalika. Karibuni nyote kwa huduma hii ya tiba.
8. KAMATI YA LAUDATO SI Kamati ya Laudato Si inatutangazia kuwa dust bins zimewekwa katika maeneo mbalimbali ya Kanisa. Tunaombwa kutupa taka tu ndani ya dust bins ili kudumisha usafi wa mazingira yetu. Tusitupe taka ovyo ovyo.
9. RATIBA YA MAFUNDISHO YA DINI
i. Ubatizo na Ekaristi ya Kwanza kwa watu wazima: Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
ii. Kipaimara: Kila Jumamosi kuanzia saa 7:00 mchana katika Ukumbi wa Mt. Agnes.
iii. Ekaristi ya Kwanza: Kila Jumapili baada ya Misa ya saa 2:00 asubuhi katika Shule ya OLOFA.



